SIMU BOMBA KWA BEI NAFUU(SAMSUNG GALAXY A70)

Nilihangaika na kukuna sana kichwa wakati nilipokuwa nikitafuta simu yenye quality nzuri ya videos na picha kwa min ajili ya YouTube channel yangu. Naam! Nilifahamu kuwa zipo simu nzuri sana zenye quality ya hali ya juu ya videos na picha ambazo zingenifaa zaidi ya sana. Hata hivyo, bei yake ilikuwa haiendani kabisa na mfuko wangu. Ni simu ghali sana ambazo aghlabu humilikiwa na mabwenyenye. Nilihuzunika sana nilipofahamu ya kwamba kwa kiwango cha pesa nlichonacho basi huenda nisipate simu muafaka kwa kazi yangu ya YouTube.

Atafutaye hachoki ebo! Baada ya kuingia katika maduka mbali mbali na kuzama mitandaoni kutafuta simu maridhawa, nilikutana na simu ambayo kwamba haikuwa tu nzuri bali pia ya bei ya chini ukilinganisha na features iliokuwa nazo. SAMSUNG GALAXY A70. Niliifanyia utafiti wa kutosha simu hii kabla ya kuinunua na niligundua kuwa ni simu yenye features nyingi nilizokuwa nikizitaka. Kwanza ina quality ya camera ajab, storage capacity kubwa, hizi features mbili niliziona kuwa muhimu katika kuifanya kazi yangu ya YouTube bila stress. Aidha ina features nyingine ambazo zilinifurahisha sana.

Features za SAMSUNG GALAXY A70

  • 6.7 inches display size
  • 128GB internal storage
  • 32mp+8mp+5mp Rear camera
  • 4,500mAh battery size

Hii simu ina ukubwa wa kufurahisha, ukiishika mkononi unaskia raha. Mimi siku hizi sina haja ya laptop kwasababu kutype, kuedit videos,yaani kila kitu natumia simu yangu ya Samsung Galaxy A70. Vile vile, hii simu ina storage kubwa sana(128GB), unaweza kuhifadhi mambo mengi sana ndani yake. Aidha,  inajaa charge haraka sana na inakaa na charge kwa muda mrefu. Camera yake nayo usiseme!

Baada ya kuinunua simu hii nilithibitisha kuwa naam ni simu bomba. Watu wengi wamenisifia videos zangu za YouTube na kusema kuwa ziko clear na quality ni nzuri sana.

Je unasubiri nini? Jinunulie Samsung Galaxy A70 leo ufurahikie features za kishua.

Bonyeza hapa?ujinunulie simu yako

SHOP NOW

Subscribe to Blog via Email

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 69 other subscribers

About Farwat Shariff

Farwata ambaye kwamba anatumia lakabu ya ashiki wa kiswahili katika uandishi wake ni kwa sasa hivi mwanafunzi wa somo la uchumi anayeishi Mombasa, Kenya. Aidha ni mjasiriamali, malenga na mwandishi wa kiswahili anayependa na aghlabu huandika kuhusu mambo yanayotokea na kuathiri jamii. Kuandika ni faraja yangu! Watu kuburudika na uandishi wangu ni furaha yangu❤

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *