AINA ZA MANENO

      3 Comments on AINA ZA MANENO

NENO NI NINI?

Neno ni kipashio kidogo zaidi kinachojihimili katika sentensi. Kiungo hiki huwakilisha maana inayokubalika katika sarufi ya lugha maalum.

Kuna aina nane kuu za maneno katika lugha ya Kiswahili.

  • Nomino (N)
  • Vitenzi (T)
  • Viwakilishi (W)
  • Vivumishi (V)
  • Vielezi (E)
  • Viunganishi (U)
  • Vihusishi (H)
  • Vihisishi (I)

NOMINO

Nomino ni maneno yanayoeleza majina ya watu, vitu, mahali, hali, tabia au taratibu. Kwa mfano, Fatma, uvivu, nyumbani.

AINA ZA NOMINO

1.NOMINO ZA KIPEKEE: Nomino ambazo hutaja vitu vya kipekee. Nomino hizi hutaja kitu kwa kukitambulisha waziwazi kwa jina au majina yake kamili. . Majina  haya huanza Kwa herufi kubwa ima iwe mwanzoni mwa sentensi au hata katikati. Nomino hizi hazina wingi. Mfano Kenya, Otieno nk.

2. NOMINO ZA JUMLA (KAWAIDA): Hizi ni nomino  zinazotaja  kitu  bila kukitambulisha kwa jina lake halisi. Kwa mfano  kama ni mji  hatuambiwi  ni Nairobi au Mombasa. Nomino  hizi huanza kwa herufi ndogo isipokuwa tu zinapotokea mwanzoni mwa sentensi. Mfano wa nomino za kawaida, nchi, kitabu, mtu, nk.

3. NOMINO ZA JAMII/MAKUNDI: Nomino za vitu vinavyotokea kwa makundi. Kila kundi hurejelewa kwa kutumia  jina au nomino  maalum. Kwa mfano, umati wa watu, tita la kuni nk.

4. NOMINO ZA WINGI: Nomino hizi hutokea tu kwa wingi.  Haziwezi kugawika ili ziwe kitu kimoja  kimoja. Kwa mfano, mazingira, maji nk.

5.NOMINO ZA DHAHANIA: Majina ya vitu vya kufirika tu wala haviwezi kugusika, kuonjeka  au kuonekana.Havina jumbo halisi. Kwa mfano, furaha, huzuni, wasiwasi nk.

6.NOMINO ZA VITENZI JINA:  Nomino zinazoundwa kutokana na vitenzi. Huundwa kwa kuongezewa kiambishi ‘ku_’ mwanzoni mwa mzizi wa kitenzi. Kwa mfano, kulima.

Jifunze VITENZI

Jifunze VIWAKILISHI

Jifunze VIVUMISHI

Jifunze VIELEZI

Jifunze VIUNGANISHI

Jifunze VIHUSISHI

Jifunze VIHISISHI

MAREJELEO

  1. Kimani Njogu na Dorothy K. Nganje, kiswahili kwa vyuo vya ualimu: Jomo Kenyatta Foundation 2006.
  2. Kimani Njogu, Alice Mwihaki na Aswani Buliba, Sarufi ya kiswahili: uchanganuzi na matumizi: Jomo Kenyatta Foundation 2006.
  3.  G. Waihiga na K.W. Wamitila, chemichemi za kiswahili kidato cha pili 2003.

3 thoughts on “AINA ZA MANENO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *