JINSI YA KUPIKA VIAZI VYA NAZI VYA NYAMA

MAHITAJI
▪Viazi kilo moja vilivyochambuliwa maganda na kukatwa slices(hakikisha slices si nyembamba Sana ili visivurugike)
▪Nyama nusu iliochemshwa na chumvi
▪Tui zito kikombe 1
▪Tui jepesi(matusha) vikombe 4
▪Tomato 4 zilizokatwa katwa au kusagwa
▪Tomato paste kijiko 1 cha kula
▪Kitunguu maji 1 kilichokatwa katwa
▪Kitunguu thomu kilichosagwa kijiko 1 cha kula
▪Dania moja iliokatwakatwa
▪ Pilipili boga 1(hoho) lililokatwa katwa
▪Carrot 1 iliokatwakatwa
▪ pilipili manga iliosagwa kijiko 1 cha chai
▪ Curry powder kijiko 1 cha kula
▪royco kijiko 1 cha kula
▪chumvi kiasi

MATAYARISHO
▪weka mafuta kwenye sufuria ubandike motoni
▪Mafuta yakishika moto, weka kitunguu maji uache kiturn golden brown
▪weka kitunguu thomu, Curry powder na pilipili manga upike Kwa sekunde kadhaa
▪weka Dania, pilipili boga na carrots upike Kwa sekunde 30
▪weka Tomato, tomato paste na chumvi ufunike uache ziive na kukauka maji Kwa takriban dakika 3
▪weka viazi, nyama na supu yake na matusha ufunike mpaka Viazi viive.(hakikisha nyama hauiachi na supu nyingi kwasababu kuna matusha)
▪Viazi vikishaiva, weka tui zito ambalo umekoroga royco ndani yake na uache Kwa dakika 1
▪Viazi vipo tayari
▪Andaa Kwa chapati, mahamri au hata vikavu pia.
▪pia unaweza ukal Viazi hivi Kwa pilipili ya ndimu

Kwa mapishi zaidi mutanipata;
? You tube@farwat’s kitchen
? Instagram@farwats_kitchen
? Facebook@farwat’s kitchen

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *