Author Archives: Farwat Shariff

About Farwat Shariff

Farwata ambaye kwamba anatumia lakabu ya ashiki wa kiswahili katika uandishi wake ni kwa sasa hivi mwanafunzi wa somo la uchumi anayeishi Mombasa, Kenya. Aidha ni mjasiriamali, malenga na mwandishi wa kiswahili anayependa na aghlabu huandika kuhusu mambo yanayotokea na kuathiri jamii. Kuandika ni faraja yangu! Watu kuburudika na uandishi wangu ni furaha yangu❤

HARUSI ZA MASHINDANO

Mwanangu ‘mepata heri, nikaha haiko mbali Harusi ya kifahari, na tena ilio ghali Nitamfanyia mwari, watu wakomeke kweli Nataka fanya harusi, iishinde ya fulani Kukopa nipo tayari, malaki mamilioni Harusi… Read more »

UMARIDADI HUFICHA UMASIKINI

Maneno ya tangu jadi, waliyanena waneni Kwetu sisi ni zawadi, tuyatie akilini Japo nyumba ya kukodi, ipambe nje na ndani Hakika umaridadi, huficha umasikini Tena ifukize udi, ingawa wa ishirini… Read more »

MASHAIRI YA METHALI

Hujipinda muungwana, uvivu hueka kando Vilivyo akapambana, akatenda kwa upendo Wala haongei sana, na kuvifanya vishindo Ada ya mja hunena, muungwana ni vitendo ashikiwakiswahili ❤️ Ni maneno ya hekima, maneno… Read more »

CHAPATI

Nawauliza wenzangu, la kimjadala swali Hakika ya swali langu, laniumiza akili Nijibuni wangu wangu, tupate jibu kamili Ni yapi maji sahihi, ya kukandia chapati ? Eti ni maji makali, yalopuliwa… Read more »

SAYARI YA KISWAHILI (SAYAKI)

Ni kitamu Kiswahili, ndugu fahamuni Utamu kama asali, umejaa ndani Wengi wanakikubali, anopinga nani? Kiswahili kitukuzwe! Tukipende Kiswahili, na tukithamini Tuwapo kila mahali, tukizungumzeni Dharau tuweke mbali, kwenye lugha hini… Read more »