JINSI YA KUPIKA MZINGA WA NYUKI

      No Comments on JINSI YA KUPIKA MZINGA WA NYUKI

Mzinga wa nyuki ni mkate wenye asili ya kiarabu. Mkate huu umepewa jina la mzinga wa nyuki kutokana na mfanano wake  baada ya kupikwa. Ni mkate unaopikwa mfano wa skonzi na kuwekwa cheese katikati ya kila skonzi na hatimaye kumwagiwa maziwa ya mgando au shira kwa juu. Ni mkate ambao kwamba licha ya kuwa rahisi kuandaa pia ni mtamu ajabu. Unaweza ukaandaa mkate huu kama kiamsha kinywa, chajio au hata kitindamlo.

MAHITAJI 

 • Unga wa ngano vikombe 2
 • Maziwa ya vuguvugu kikombe 1
 • Sukari 2tbspns
 • Hamira 1tbspn
 • Baking powder 1/2tspn
 • Siagi 1tbspn
 • Cheese
 • Maziwa ya mgando
 • Ufuta (sio lazima)

MATAYARISHO 

 • Weka unga, siagi, sukari, baking powder na hamira. Kisha weka maziwa kidogo kidogo ukiendelea kukanda

 • Kanda unga mpaka uchanganyike na ukandike vizuri na pia hakikisha unga unakuwa laini kuliko unga wa chapati.
 • Funika unga uache uumike kwa takriban dakika 30 kutegemea na temperatures.

 • Baada ya unga kuumuka tengeneza maduara madogo madogo na ueke cheese kwenye kila donge
 • Zipangilie vizuri kwenye sehemu yako ya kuoka na uziache tena kwa takriban dakika 10.
 • Baada ya dakika kumi paka yai juu na umwagilie ufuta juu
 • Oka kwa takriban dakika 20 kwa moto wa 180°C. Unaweza pia ukatumia jiko la makaa.
 • Baada ya hapo zipo tayari

 • Baada ya mkate kuwa tayari, mwagia maziwa ya mgando kwa juu mkate ukiwa bado u moto.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *