JINSI YA KUPIKA KEKI YA CHOCOLATE TAMU SANA NA RAHISI KWA KUTUMIA BLENDER

Keki ya chocolate ni keki inayopendwa sana. Wengine wananunua au kuweka oda jambo ambalo kwamba ni la gharama kuliko kuoka mwenyewe nyumbani. Wengine wanawazawadi wendani wao keki walizonunua, jambo ambalo kwamba bila  shaka linapendeza sana. Hata hivyo,  utakubaliana nami kuwa kumzawadi mtu kitu ulichokitengeneza kutumia mikono yako inapendeza zaidi. Hivyo basi, nitawaelezea jinsi ya kuoka keki ya chocolate kwa njia rahisi sana na utaweza kuwaandalia uwapendao na kuweka tabasamu kwenye nyuso zao.

Nikiwa mkweli zaidi, miongoni mwa keki nilizowahi kupika basi hii ilikuwa bomba. Resipe hii ni rahisi sana kuitumia na kuikumbuka vile vile. Ikiwa unahitaji resipe ya keki isiokuwa na mambo mengi na yenye kueleweka kiurahisi zaidi, basi bila shaka hii itakufaa.

MAHITAJI 

 • Mayai 6
 • Blueband ya kupima robo(1/4kg)
 • Unga robo (250g)
 • Sukari robo (250g)
 • Cocoa 40g
 • Baking powder kijiko kimoja cha mezani (1tbspn)

MATAYARISHO

 • Kama unatumia jiko la makaa, washa jiko liendelee kushika pole pole.
 • Tayarisha sufuria yako ya kuokea keki kwa kueka karatasi chini na kupaka siagi ili iwe rahisi keki kutoka itakapoiva.
 • Weka mayai, sukari na blueband kwenye blender ublend kwa takriban dakika kumi

 • Mimina mchanganyiko kwenye bakuli
 • Gawanya unga mafungu matatu
 • Weka unga kwenye mchanganyiko fungu baada ya fungu huku ukichekachekecha kisha ukoroge vizuri. Endelea kufanya hivyo mpaka mafungu yaishe.(kuchekecha unga inasaidia mavumbo ya unga kubaki juu.Na kuweka unga fungu baada fungu inasaidia unga kukorogeka vizuri zaidi)

 • Weka baking powder uchanganye vizuri
 • Weka cocoa pia uchanganye vizuri

 • Mimina kwenye sufuria na uoke kwa kutumia jiko la makaa. Ifunike keki yako na ueke makaa juu na kwenye jiko ubakishe makaa kidogo sana. Hakikisha juu hueki makaa mengi sana ili keki yako isiungue. (Unaweza ukatumia oven)
 • Oka kwa takriban dakika 40_50
 • Weka kijiti ndani na kikitoka kikavu basi keki ipo tayari.

3 thoughts on “JINSI YA KUPIKA KEKI YA CHOCOLATE TAMU SANA NA RAHISI KWA KUTUMIA BLENDER

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *