VITENZI

      No Comments on VITENZI

VITENZI 

Vitenzi ni maneno yanayoarifu kuhusu jambo linalotendwa au kutendewa nomino. Vitenzi huwa na mzizi ambao kwamba ndio unaosimamia tendo lenyewe na mzizi huo huambatanishwa na viambishi ili kuleta maana inayokusudiwa. Kwa mfano, alipita.

A-li-viambishi awali

pit-mzizi 

a- kiambishi tamati

AINA ZA VITENZI 

1.VITENZI HALISI(T): Vitenzi hivi huonyesha kitendo halisi, kikubwa au muhimu kilichotendwa na mtendaji. Kwa mfano, mama anapika pilau.

2. KITENZI KISAIDIZI(Ts): ni kipengele cha neno au maneno kinachosaidiana na kitenzi kikuu ili kitendo kilichotendwa kifafanuliwe au kieleweke zaidi. Kwa mfano, mwalimu alikuwa anafunza hisabati.

3. KITENZI KISHIRIKISHI(t): Vitenzi vinavyoshirikisha vitu kihali, kitabia au kimazingira. Kwa mfano:

 • Khalid ni mvulana mtiifu.
 • Mwalimu wetu si mkali.
 • Yule ndiye mwanafunzi aliyeibuka wa kwanza.
 • Sisi tu mabinti wenye msimamo.

Vitenzi vishirikishi ni vya aina mbili:

a) Vitenzi vishirikishi vikamilfu: Hivi vinaweza kuchukua viwakilishi nafsi au viambishi vya ngeli na pia viambishi vya wakati. Ni maneno kama, weza, kuwa, kwisha, kuja, taka, ngali, pasa, bidi, pata na kwenda. Kwa mfano:

 • Mtoto amekuwa kwa shangazi yake.
 • Kijana yule anapaswa kuwa hospitalini.

Vitenzi vishirikishi vikamilifu mara nyingine huweza kutokea kama vitenzi visaidizi iwapo vinatokea sambamba na vitenzi vikuu. Kwa mfano:

 • Mpishi alikuwa anapika.

b)Vitenzi vishirikishi vipungufu: vitenzi hivi haviwezi kuchukua viambishi vya wakati ingawa vinaweza kuchukua viwakilishi nafsi viambata au viambishi nngeli.kwa mfano:

 • Sharifa ni msichana mrembo.
 • Yule si mtoto mtukutu.
 • Gari li maegeshoni.
 1. Kimani Njogu na Dorothy K. Nganje, kiswahili kwa vyuo vya ualimu: Jomo Kenyatta Foundation 2006.
 2.  G. Waihiga na K.W. Wamitila, chemichemi za kiswahili kidato cha pili 2003

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *