VIELEZI

      No Comments on VIELEZI

VIELEZI

Vielezi ni maneno yanayotumika kufafanua kitenzi, kivumishi au kielezi kingine.

Au pia, ni maneno yanayosifu au kufasili sura za vitenzi, vivumishi au vielezi vingine.

Vielezi vinapotumika kufafanua vitenzi 

  • Mtoto yule alianguka vibaya. 

vielezi vinapotumika kufafanua vivumishi

  • Chakula alichopika mama ni kitamu sana

vielezi vinapotumika kufafanua vielezi vingine 

  • Mpishi yule alipika chakula vizuri sana

AINA ZA VIELEZI 

1. VIELEZI VYA NAMNA: Hivi huonyesha namna kitendo kinavyotendeka. Hujibu swali “vipi?”. Kwa mfano,  nyanya alitembea taratibu. 

2. VIELEZI VYA MAHALI: Hivi huonyesha mahali kitendo kinapotokea au kutendeka. Kwa mfano,  mama alikwenda sokoni. Alipanda Juu ya mti akaangua machungwa.

3. VIELEZI VYA WAKATI: Hivi hueleza wakati wa kutendeka kwa kitendo. Kwa mfano,  alichapisha kitabu chake mwaka jana. 

4. VIELEZI VYA IDADI: Vielezi hivi hueleza kiasi cha kutendwa kwa tendo flani. Pia vielezi hivi huonyesha ni mara ya ngapi katika safu kitendo kimefanyika. Kwa mfano,  ameenda sokoni mara tatu leo.

5. VIELEZI VIINGIZI: Vielezi hivi huiga jinsi kitendo kilivyotendwa. Hufafanua vitenzi kwa kufuatanisha mlio baada ya kitendo kutendeka. Kwa mfano, mtoto alilala fofofo! 

6.VIELEZI VIULIZI: Vielezi hivi huuliza juu ya tendo. Kwa mfano,  utakuja lini kututembelea?

7. VIELEZI VIONYESHI: Hivi hutumiwa kuonyesha mahali tendo lilifanyika. Kwa mfano,  alienda pale kununua viazi.

MAREJELEO

  1. Kimani Njogu na Dorothy K. Nganje, kiswahili kwa vyuo vya ualimu: Jomo Kenyatta Foundation 2006.
  2. Kimani Njogu, Alice Mwihaki na Aswani Buliba, Sarufi ya kiswahili: uchanganuzi na matumizi: Jomo Kenyatta Foundation 2006.
  3.  G. Waihiga na K.W. Wamitila, chemichemi za kiswahili kidato cha pili 2003

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *