JINSI YA KUPIKA PILAU YA KUKU

      7 Comments on JINSI YA KUPIKA PILAU YA KUKU

Pilau ni chakula maarufu sana katika sehemu nyingi ulimwenguni. Aidha ni chakula kinachopendwa na kuenziwa na wengi, si wakubwa si wadogo. Bila shaka pilau inapendwa kutokana na sifa zake sufufu. Kwanza kabisa ni chakula chenye ladha marua. Vile vile ni chakula rahisi sana kutayarisha na kinachukua muda mchache sana kuwa tayari. Licha ya yote hayo, ni chakula kinachohitaji viungo vya kawaida sana vinavyopatikana katika soko lolote lile.

Naam, mapishi ya pilau bila shaka ni mengi. Wapo wanaopika pilau ya kawaida au wengine wanapenda kuipamba kwa njegere, zabibu au viungo vingenevyo. Huenda viungo vinavyotumika vikawa sawa lakini wakati wa kuviweka viungo hivyo ikaleta tofauti ya ladha. Au pia wengine wanaweza wakatumia viungo aina nyingi zaidi kuliko wengine na ndipo pia tofauti ya ladha inapojitokeza.

MAHITAJI 

 • Mchele 1/2 kg(nusu kilo)
 • Kuku mmoja wa kiasi aliyekatwa katwa na kuoshwa vizuri
 • Vitunguu maji 2 vilivyokatwa katwa slices
 • Pilipili boga 1
 • Karoti 1
 • Dania 1
 • Tomato/nyanya 2 zilizokatwa katwa au kublendiwa
 • Viazi 3 vilivyokatwa katwa
 • Tomato paste/nyanya ya mkebe vijiko 2 vya mezani
 • Kitunguu thomu kijiko 1 cha mezani
 • Kijiko 1 cha chai mdalasini iliopondwa
 • Kijiko 1 cha chai pilipili manga iliopondwa
 • Kijiko 1 cha chai bizari nyembamba iliopondwa
 • Mafuta uto/mafuta ya kupikia takriban vijiko 3 vya mezani

MATAYARISHO 

 • Marinate kuku (weka siki na chumvi kwenye kuku umuache kwa takriban nusu saa)
 • Bandika sufuria motoni ueke mafuta, yakishika moto weka kitunguu ukikaange mpaka kiwe hudhurungi (golden brown)

 • Weka spices zote(dawa za pilau) pamoja na kitunguu thomu upike kwa sekunde kadhaa
 • Weka tomato, pilipili boga , karoti ,tomato  paste na kuku ufunike uache ziive kwa takriban dakika 10

 • Weka mchele uupike kwa sekunde kadhaa
 • Weka viazi na maji kiasi. funika mpaka maji yaelekee kukauka, takriban dakika 10(kiasi cha maji itategemea na mchele. Mimi nimetumia sunrice kwa hiyo nimeweka maji kiasi cha kufunika mchele na kuzidi kidogo)
 • Weka dania ukoroge vizuri na uyaache maji yakauke vizuri

 • kisha ufunike uweke moto mdogo kabisa kama unatumia gas cooker kwa takriban dakika 10_15(kama unatumia jiko la makaa weka moto wa juu na chini)

 • Pilau ipo tayari

 • Andaa kwa  kachumbari , pilipili ya kukaanga na juice ya maembe

7 thoughts on “JINSI YA KUPIKA PILAU YA KUKU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *