JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA MAPAPAYU

      No Comments on JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA MAPAPAYU

Naam, yapo mapishi mengine yanaweza yakawashtua wale ambao kwamba hawayajazoea au hawajahi yaskia. Bila shaka tambi za mapapayu ni miongoni mwa mapishi hayo. Hata hivyo, tambi za mapapayu ni chakula maarufu sana katika kanda ya pwani na aghlabu huandaliwa wakati wa ramadhan. Vile vile ni chakula kitamu sana ambacho kwamba binafsi ninakienzi. Ila swali ni je, ni nani aliyekaa akafikiria na kutunga chakula hichi? Bila shaka atakuwa mbunifu mbuji.

Leo hii nitawaelezea jinsi ya kupika tambi za mapapayu zilizopikwa kwa nazi na sukari. Sio siri kama wewe ni mgeni wa mapishi haya huenda ukashangaa ni majanga gani watu wengine wanapika lakini yajaribu tu na nina imani utazama kwenye wingu la mapenzi na mapishi haya kuntu kuntuba.

MAHITAJI 

 • Tambi za mapapayu (papayu lilokatwa maganda na kukatwa kwa urefu kama tambi) kiasi bakuli moja la kiasi
 • Tui zito kikombe 1
 • Tui jepesi kikombe 1&1/2
 • Sukari  kikombe 1
 • Iliki kiasi

MATAYARISHO 

 • Weka tambi kwenye  sufuria na  maji kiasi cha kufunika tambi, zifunike na uziache zichemke mpaka ziive(zibonyeze na ukiziona ziko laini basi zimeiva) Tambi nyingine ni cherema na huenda zikachukua muda mrefu zaidi kuiva
 • Kisha mwaga maji ya ziada

 • Weka sukari, tui jepesi na iliki kwenye zile tambi ulizozimwaga maji na urejeshe motoni kwa takriban dakika 10

 • Kisha weka tui zito na uziache motoni kwa takriban dakika 5

 • Baada ya hapo tambi zipo tayari
 • Andaa mezani kwa chai ya mkandaa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *