JINSI YA KUPIKA TAMBI NA NYAMA YA KUSAGA_SPAGHETTI

Tambi, maarufu kama spaghetti kinaaminika kuwa chakula chenye asili ya kiitaliano. Hapa nchini kenya,kwa uchunguzi wangu wa haraka  haraka  nimegundua kuwa tambi ni chakula kinachopendwa sana na wasomali. Naam, Mapishi ya tambi yapo ya aina tofauti tofauti, kuanzia tambi za sukari na za chumvi ambazo kwamba aghlabu huandaliwa kwa nyama ya kusaga. Hata hivyo, wapo wengine wanaoandaa tambi kwa mchuzi wa viazi au hata mayai.

Leo nitawaelezea jinsi ya kupika tambi tamu sana pamoja na nyama ya kusaga. Tambi zetu za leo ni tambi zilizopikwa kwa kukolezwa nyanya ya mkebe pamoja na karoti na pilipili boga ili zipate ladha nzuri na muonekano mzuri wa uwekundu uwekundu na sio ziwe nyeupe kama mzungu. Muonekano  wa chakula  ni muhimu sana  japo wengine  watakwambia  bora ladha na chakula  kifike tumboni. Kuteremshia tambi zetu ni nyama ya kusaga iliopikwa kwa njia flani rahisi na kutupiwa tupiwa majani ya gilgilani kwa juu.

MAHITAJI 

TAMBI

 • Spaghetti  450g
 • Kitunguu maji 1
 • Pilipili boga 1 lilokatwa kwa urefu
 • Karoti 1 ilokatwa kwa urefu
 • Chumvi kiasi

NAMA YA KUSAGA 

 • Nyama ya kusaga (kima) robo
 • Tomato/nyanya 4 zilizosagwa
 • Nyanya ya mkebe kijiko 1 cha mezani
 • Viazi 3 vilivyokatwa katwa vidogo vidogo (cubes)
 • Kitunguu maji 1 kilichokatwa katwa
 • Pilipili boga 1
 • Karoti 1
 • Dania 1
 • Kitunguu thomu vijiko 2 vya mezani
 • Pilipili manga kijiko 1 cha chai
 • Mdalasini kijiko 1 cha chai
 • Karafuu kidogo
 • Curry powder kijiko 1 cha mezani
 • Chumvi kiasi

MATAYARISHO (TAMBI)

 • Bandika maji motoni ueke chumvi na ufunike
 • Yakichemka weka tambi ukizivunja vunja

 • Tambi zikishaiva mwaga maji yaliobaki uzieke pembeni
 • Kwenye sufuria, weka mafuta
 • Mafuta yakishika moto, weka kitunguu ukipike kwa sekunde chache (kiwe translucent)
 • Weka karoti na pilipili boga pia upike kwa sekunde kadhaa
 • Weka nyanya ya mkebe uipike kwa sekunde kadhaa (unaweza ukaongeza chumvi kama kwenye tambi haikutokea)

 • Kisha weka tambi ulizozichemsha ukoroge mpaka zichanganyike vizuri

 • Tambi zipo tayari! Tuanze matayarisho ya nyama ya kusaga

MATAYARISHO YA NYAMA YA KUSAGA 

 • Weka nyama kwenye sufuria na ueke kitunguu  thomu  nusu ya lile ulichosaga, pilipili manga, mdalasini na chumvi

 • Ichanganye vizuri ubandike motoni mpaka iive na maji yote yakauke(hakikisha unaibonda bonda ili isiwe madonge madonge)
 • Weka pembeni
 • Kwenye sufuria nyingine, weka mafuta ta kupikia
 • Yakishika moto weka karafuu upike kwa sekunde kadhaa
 • Kisha weka kitunguu maji ukipike mpaka kiwe golden brown
 • Weka kitunguu thomu na curry powder
 • Weka nyama ukoroge vizuri
 • Weka pilipili boga, carrot, tomato, viazi, tomato ya mkebe na chumvi

 • Funika upike kwa moto mdogo mdogo mpaka viazi viive
 • Weka dania (majani ya gilgilani)

 • Msosi wetu upo tayari
 • Weka zile tambi kwenye sahani na ueke hii nyama kwa juu
 • Andaa kwa sharubati ya maembe

2 thoughts on “JINSI YA KUPIKA TAMBI NA NYAMA YA KUSAGA_SPAGHETTI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *