JINSI YA KUPIKA MCHICHA WA NAZI

      No Comments on JINSI YA KUPIKA MCHICHA WA NAZI

Mchicha ni mboga tamu sana lau itapikwa kwa njia muafaka. Ni mboga ambayo kwamba inaendana na vyakula aina tofauti tofauti hususan wali au ugali. Inapendeza zaidi ikiwa pembeni kutakuwa na samaki wa kukaanga, kuku au hata nyama. Mapishi ya mchicha yapo aina tofauti tofauti lakini mchicha ninaoupenda zaidi ni mchicha wa nazi. Hivi ninavyoandika mate yamenijaa mdomoni nusura kudondoka. Navuta taswira ya ugali, mchicha uliokolea nazi na samaki wa kukaanga bila kusahau achari ya maembe. Tusidondoke mate sana, ungana nami tujifunze mapishi haya ili upikie familia wafurahie.

 

MAHITAJI 

 • Mchicha ulioshwa vizuri na kukatwa katwa
 • Viazi 3 vilivyokatwa vidogo vidogo (cubes)
 • Nyanya 4(tomato) zilizokatwa vipande vidogo vidogo
 • Carrot 1,pilipili boga 1, kitunguu maji 1 na dania 1 zilizokatwa katwa
 • Thomu iliosagwa na tangawizi kijiko 1 cha mezani
 • Matusha(tui jepesi) kikombe 1
 • Tui zito kikombe 1
 • Chumvi kiasi
 • Curry powder kijiko 1 cha mezani
 • Royco kijiko 1 cha mezani

MATAYARISHO 

 • Bandika mafuta ya kupikia takriban vijiko 3 vya mezani na yakishika moto weka kitunguu maji. Kitunguu kikigeuka hudhurungi (golden brown) weka kitunguu thomu na curry powder upike kwa sekunde kadhaa. Kisha weka pilipili boga, carrot na dania pia uzipike kwa sekunde kadhaa. Kisha weka tomato na chumvi

 • Koroga vizuri na ufunike mpaka tomato ziive vizuri.
 • Weka mchicha na viazi ufunike mpaka viazi viive

 • Viazi na mchicha ukishaiva, weka tui jepesi upike kwa dakika takriban mbili.
 • Hatimaye, weka tui zito ambalo kwamba ndani umekorogea royco na upike kwa sekunde 2 hivi

 • Baada ya hapo, mchicha upo tayari.
 • Andaa kwa ugali au wali na samaki wa kukaanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *