JINSI YA KUPIKA MKATE WA NYAMA(MEAT CAKE)

      No Comments on JINSI YA KUPIKA MKATE WA NYAMA(MEAT CAKE)

Kwa muda mrefu sana mama yangu amekuwa akinirai nipike mkate huu wa nyama. “Farwa chukua video ya mkate wa nyama ueke YouTube, watu wataipenda.” Huu ulikuwa wimbo wa mama yangu kwa siku nyingi lakini maneno yake yaliingia kwenye sikio langu la kulia na kutokea kwenye sikio la kushoto😂Alafu ilkuwa nashuku ni kama alikuwa ametamani mkate wa nyama kisha anatumia YouTube kama kisingizio 😂😂😂Hata hivyo, ilifika siku nikaamua tu mwenyewe niupike mkate huu. Kiukweli ilikuwa mara yangu ya kwanza kuutayarisha na nilipendezwa mno na utayarishaji wake pamoja na ladha yake murua. Ni chakula ambacho kwamba ni rahisi sana kupika na mahitaji yake pia ni ya kawaida. Hatimaye mama yangu alikata kiu yake ya mkate wa nyama 😅❤

MAHITAJI 

 • Nyama ya kusaga 1/2kg
 • Mayai 6
 • Tomato 1 iliokatwa slice
 • Carrot 1 kubwa iliokatwa kwa urefu na nyembamba nyembamba
 • Pilipili boga 1 iliokatwa kwa urefu
 • Vitunguu maji 2 vilivyokatwa vidogo vidogo
 • Maji ya limau/ndimu 1
 • Kitunguu thomu kilichosagwa na tangawizi kijiko 1 cha mezani
 • Pilipili manga kijiko 1 kidogo
 • Mdalasini kijiko 1 kidogo
 • Chumvi kiasi

MATAYARISHO 

 • Weka kitunguu thomu, pilipili manga, mdalasini, maji ya limau/ndimu na chumvi kwenye nyama na uchanganye vizuri. Bandika nyama motoni,ifunike na uipike kwa moto mdogo mdogo mpaka iive na maji yote yakauke

 • Weka kitunguu maji chote na carrot nusu yake uchanganye vizuri

 • Kwenye bakuli weka mayai na chumvi kidogo upige kwa mchapo  mpaka yachanganyike vizuri

 • Weka mayai kwenye ile nyama uloweka vitunguu na carrot na uchanganye vizuri. Kisha paka sufuria nyingine mafuta chini na pembezoni kisha weka mchanganyiko wa nyama kwenye sufuria hiyo. Kupaka mafuta kwenye sufuria kunasaidia mkate usishike chini wakati wa kubake ili iwe rahisi kuutoa ukiiva
 • Pangalia tomato, pilipili boga na carrot juu ya mchanganyiko wa nyama. Hii inasaidia kuleta muonekano mzuri na pia ladha.

 • Bake kwa moto wa 250°C kwa takriban dakika 10_15(unaweza ukapika kwa moto wa juu na chini kwenye jiko la makaa) Kupika mkate huu hakuhitaji muda mwingi kwasababu nyama imeiva, kinachohitajika ni mayai tu kushikanisha mkate
 • Mkate upo tayari. Kata vipande vipande uandae kwa juice ya maembe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *