JINSI YA KUPIKA KUKU WA KUOKA MTAMU SANA NA KWA NJIA RAHISI

Kuku ni chakula kinachopendwa na wengi kote ulimwenguni. Kenya, watu wanaokienzi kitoweo cha kuku ni wenzetu kutoka sehemu ya magharibi, waluhya😅. Vile vile, kuku anaweza kumtia mtu kwenye matatizo😱. Wapo mabinti wakinunuliwa tu vibanzi na kuku ni rahisi sana kuingia kwenye mtego wowote mbele yao. Hii inadhihirisha ni kiasi gani kitoweo cha kuku kinavyopendwa na kuthaminiwa. Naam, yapo mapishi aina aina ya kuku. Si kuku wa kuchemsha,  si wa kukaanga,si wa kuchoma,si kuku wa KFC, si mchuzi wa kuku miongoni mwa mapishi mengineo .Utakubaliana nami kuwa kuku akichemshwa na chumvi tu ni mtamu seuze akipikwa kwa njia muruwa. Ili kuona mapishi ya pizza ya kuku, bonyeza  hapa.

Ungana nami tujifunze jinsi ya kupika kuku mtamu sana na kwa njia rahisi.

MICROWAVE OVEN. SHOP NOW👇

MAHITAJI 

 • kuku 1 aliyekatwa vipande vipande na kukoshwa vyema
 • Maziwa mala/mtindi kikombe 1
 • Kitunguu thomu kilichosagwa kijiko 1 cha mezani
 • Tangawizi iliosagwa kijiko 1 cha mezani
 • Chicken masala kijiko 1 kidogo
 • Paprika kijiko 1&1/2cha mezani
 • Dania ya unga kijiko 1 kidogo
 • Pilipili manga kijiko 1 kidogo
 • Mafuta ya kupikia vijiko 2 vya mezani
 • Chumvi kiasi
 • Limau/ndimu 1

MATAYARISHO

 • Weka mahitaji yote kwenye kuku. (Unaweza ukachanganya mahitaji yote kwenye maziwa mala pia)

 • Changanya kila kitu vizuri kisha funika uache kwa takriban saa 1 ili viungo viingie ndani ya kuku vizuri.

 • Bake kuku kwenye oven kwa moto wa 250°C kwa takriban saa 1.
 • Pia unaweza ukamchoma kwa makaa ukaweka moto wa juu na chini. Hakikisha moto wa juu ni mwingi kuliko moto wa chini.
 • Ukiona baada ya muda huo kuku bado hajakauka vizuri basi unaweza ukaongeza muda.

 • Kuku yupo tayari.
 • Andaa mezani kwa chipsi au wali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *