JINSI YA KUPIKA PILAU YA PAPA MKAVU

      No Comments on JINSI YA KUPIKA PILAU YA PAPA MKAVU

Pilau ni chakula maarufu sana katika kanda ya pwani na ulimwenguni kwa jumla. Utakubaliana nami kuwa ni chakula kilichojinyakuli nafasi kuntuba katika nyoyo za wengi. Ni nadra sana uende katika shughuli flani, ima harusi au matanga ukose pilau miongoni mwa vyakula vilivyoandaliwa na hili aghlabu hutokea sehemu kama Mombasa, Kenya. Hivi unajua ni kwa  nini? Ni kwasababu pilau ni chakula cha haraka haraka sana kuandaliwa, kinahitaji gharama ndogo na licha ya hayo, kinapendwa na takriban kila mtu.
Naam, kama wasemavyo mchele mmoja mapishi ni mengi. Pilau vile vile ina mapishi mengi kama mchanga wa baharini. Kuna pilau ya nyama ya mbuzi, ya nyama ya ngombe, ya kuku, ya kamba, ya samaki,  ya papa mkavu na pilau njeri🤣. Pengine zipo aina nyingine za pilau ambazo sijazitaja. Kama unazifahamu dondosha comment.Je
Pesa hazitoshi kununua nyama na umetamani kula pilau murua na tamu? Usikune kichwa kwani leo nitawaelezea jinsi ya kupika pilau ya papa mkavu tamu sana. Kama tunavyofahamu, papa wakavu ni rahisi sana, takriban shilingi kumi kwa kipande kimoja. Hivyo basi kaa makini ujifunze mapishi haya.

MAHITAJI 

 • Mchele nusu kilo(1/2kg)
 • Papa vipande 5
 • Viazi 3 vilivyokatwa katwa
 • Tomato 4 zilizokatwa katwa
 • Tomato ya mkebe(tomato paste) kijiko 1 cha mezani (sio lazima)
 • Kitunguu maji 2 vilivyokatwa katwa
 • Dania 1
 • Pilipili boga 1 lililokatwa
 • Kitunguu thomu kilichosagwa kijiko 1 cha mezani
 • Pilipili manga kijiko 1 cha chai iliopondwa
 • Mdalasini kijiko  1 cha chai iliopondwa
 • Bizari nyembamba/ jira kijiko 1 cha chai iliopondwa

MATAYARISHO

 • Kanga kitunguu maji mpaka kigeuke hudhurungi

Kikibadilika rangi ya hudhurungi, weka pilipili manga, mdalasini, jira na upike kwa sekunde kadhaa. Kisha weka pilipili boga pia upike kwa sekunde 30 na baada ya hapo weka tomato na ufunike kwa takriban dakika 10 mpaka tomato ziive

 • Weka maji ufunike mpaka yachemke(kiasi cha maji itategemea na aina ya mchele unaoutumia).maji yakichemka weka mchele, Viazi na papa. Funika mpaka maji yakauke ila usiyaache yakauke sana

 • Hatimaye weka dania ukoroge vizuri . funika upunguze moto uwe mdogo kabisa (kama unatumia gas cooker) na kama unatumia makaa toa makaa kwenye jikoubakishe kidogo sana, weka makaa kwenye kitasa ulichofunikia sufuria na cache kwa takriban dakika 10_20

 • Baada hapo pilau ipo tayari. Andaa mezani kwa pilipili ya kukaanga au achari ya maembe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *