JINSI YA KUPIKA MCHUZI WA KABABU

Je umechoka kula chapati kwa maharagwe na unahitaji kitu cha tofauti? Au pengine umepata wageni na unataka kuwapikia mapishi tofauti na yale yaliozoeleka sana? Naam, mapishi haya ya mchuzi wa kababu, ni mapishi ya kipekee ambayo abadan hayatakusinya. Ni chakula unachoweza kupika na kila mtu akakifurahikia. Vile vile ni mapishi rahisi sana kueleweka na ni vigumu sana kwa mwenye kuyapika kukosea hata kama ni mara yake ya Kwanza kuyajaribu. Ungana nami hadi mwisho ili kufahamu kinaga naga utayarishaji wa chakula hiki cha kukata na shoka.

 

MAHITAJI

 • Nyama ya kusagwa (kima) nusu kilo
 • Kitunguu maji 1 kilichokatwa katwa (cha mchuzi)
 • Vitunguu maji 3 vilivyogretiwa(vya nyama)
 • Dania mbili(ya nyama na mchuzi)
 • Pilipili boga 1 lililokatwa katwa
 • Kitunguu thomu kilichosagwa vijiko 3 vya mezani
 • Tomato 5 zilizosagwa
 • Tomato paste vijiko 2 vya mezani
 • Ndimu/limau 1
 • Pilipili manga vijiko 2 vya mezani
 • Currypowder vijiko 2 vya mezani
 • Sambhar masala vijiko 2 vya mezani
 • Mdalasini vijiko 2 vya mezani
 • Beef masala kijiko 1 cha mezani
 • Dania ya unga kijiko 1 cha mezani
 • Chumvi kiasi

JINSI YA KUTAYARISHA

 • Weka pilipili manga, currypowder, mdalasini, beef masala, dania ya unga(zote Kijiko kimoja kimoja cha mezani), Kitunguu maji kilichosagwa,dania moja,  Kitunguu thomu nusu na ubakishe nusu cha mchuzi,chumvi na ndimu na uchanganye vizuri

 • Ikishachanganyika vizuri, tengeneza shape ya kababu uzipange vizuri kwenye sufuria. Zifunike na uzipike Kwa takriban dakika 10_15

 • Zikishakauka maji ziweke pembeni uendelee na matayarisho ya mchuzi. Mate yameanza kukudondoka? Yaani ndio mwanzo mkoko unaalika maua😊Tuendelee……

 • Weka sufuria ulotia mafuta uto motoni mpaka yashike moto kisha weka Kitunguu maji ukikaange mpaka kiwe golden brown
 • Weka Kitunguu thomu, pilipili manga, currypowder na sambhar masala uzipike Kwa sekunde kadhaa
 • Weka pilipili boga na dania uzipike Kwa sekunde kadhaa
 • Weka tomato, tomato paste na chumvi ufunike Kwa dakika 5_10 mpaka tomato ziive na zikauke

 • Weka kababu uziache Kwa dakika 1

 • Mchuzi wa kababu upo tayari. Kama munavoona muonekano wake unavutia basi ladha yake ipo vivyo hivyo. Ladha muruwa itakayokuacha ukijiramba vidole. Tahadhari usijing’ate😂
 • Andaa mezani Kwa chapati na chai masala

KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA

 • Instagram@farwats_kitchen
 • Facebook@farwat’s kitchen
 • You tube@farwat’s kitchen

❤❤❤

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *