JINSI YA KUPIKA CHIPS MASALA

      No Comments on JINSI YA KUPIKA CHIPS MASALA

Vibanzi au chips kama wengi wanavyozifahamu, ni chakula maarufu, rahisi kupika, kinachopendwa na wengi ulimwenguni na zuri zaidi ni kuwa ni chakula ambacho hakipigani na mfuko wako. Hata ukijiskia kwenda kujivinjari katika mkahawa wa kifahari na pesa ulizo nazo ni kidogo basi unaweza ukaenda bila wasiwasi na kuagiza chips tu kwasababu ndicho chakula cha bei rahisi na wengi wanaweza kukimudu. Naam, hata watoto wakijua leo nyumbani kunapikwa chips basi wanakuwa na furaha ya ajabu. Wengi wetu kila tukienda mkahawani tutaiangalia menu mara mbili mbili lakini hatimaye tutaagiza kile kile tunachoagiza kila siku, chips!

Naam, chips ni chakula kitamu lakini ili kuongeza utamu huo uwe maradufu basi ni vyema kujaribu mapishi haya ya chips masala. Kuna njia tofauti tofauti za kupika chips masala na leo tutajifunza njia mojawapo ninayoipenda zaidi kwasababu ni rahisi na matokeo yake ni muruwa.

MAHITAJI

 • Viazi kilo moja vilivyokatwa kama chips
 • Tomato 4 zilizokatwa katwa/zilizosagwa
 • Kitunguu maji 1 kilichokatwa katwa
 • Pilipili boga 1/2 au 1 dogo lililokatwa katwa
 • Dania moja
 • Kitunguu thomu kijiko 1 cha mezani
 • Pilipili manga kijiko 1 kidogo iliosagwa
 • Currypowder kijiko 1 kidogo
 • Sambhar masala kijiko 1 kidogo (sio lazima)
 • Tomato ya mkebe (tomato paste) vijiko 2 vya mezani
 • Pilipili ya unga(masala) sio lazima
 • Mafuta ya kupikia (uto)

MATAYARISHO

 • Bandika mafuta kwenye karai na yakishika moto weka chips uzikange. Hakikisha zinakuwa kavu kwasababu chips kavu ndizo nzuri Kwa mapishi ya chips masala. Zikishaiva zitoe kwenye mafuta uziweke pembeni uendelee na matayarisho mengine.

 • Weka sufuria ulotia mafuta uto motoni na yakishika moto weka Kitunguu maji ukikaange mpaka kiwe golden brown
 • Weka pilipili manga, currypowder na Kitunguu thomu uzipike kwa sekunde kadhaa
 • Weka pilipili boga na dania upike Kwa sekunde kadhaa
 • Weka tomato, tomato paste na chumvi ufunike Kwa dakika 5-7 mpaka tomato ziive

 • Weka chips uchanganye vizuri. Hakikisha unachanganya kwa makini ili chips zisibondeke/zisivurugike

 • Chips masala zipo tayari. Andaa mezani kwa juisi ya maembe

KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA

 • Instagram@farwats_kitchen
 • Facebook@farwat’s kitchen
 • YouTube@farwat’s kitchen

❤❤❤

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *