
Ndizi ni tunda ninalolipenda kuliko matunda yote duniani. Ni tunda ambalo kwamba ninaweza kulila hata nikiwa mgonjwa wakati hamu ya vyakula ikiwa imetoweka. Siku kukiwa na sherehe flani nyumbani na kukinunuliwa ndizi za Kula wakati wa mchana, basi mimi nitakula takriban asilimia thelathini ya ndizi hizo. Naam, kwa upande mwingine kuna parachichi, tunda ambalo kwamba sina mapenzi nalo kwa kweli. Hata hivyo, ndizi inapochanganywa na ovacado basi natokea kuyapenda matokeo yake.
Pamoja na tunda la parachichi kuweza kutengeza kinywaji kitamu ajabu pia lina faida ndani ya mwili wa binadamu. Kwanza, tunda hili Lina virutubisho ainati zikiwemo vitamini zaidi ya aina ishirini na madini. Aidha, parachichi Lina potasiamu nyingi zaidi kuliko ndizi. Potasiamu ni mdanj ambayo kwamba ni muhimu sana yanayosaidia kuweka viwango vya shinikizo la damu kuwa Sawa. Faiba ni kirutubisho kingine kinachopatikana katika parachichi ambacho kwamba ni muhimu vile vile. Kwale walio na hamu ya kupunguza uzito wa mwili basi ulaji wa parachichi unaweza ukawatatulia shida hiyo. Naam, hizo ni faida chache miongoni mwa nyingi zinazopatikana katika tunda hili. Zipo njia nyingi za Kula tunda hili na leo leo tutajifunza njia mojawapo.
Wakati kama huu wa joto, ni vyema kupata kinywaji baridi kilichotengezwa kikatengezeka ili ujiburudishe. Kinywaji cha parachichi ni kinywaji kilicho na ladha ya kipekee ambayo kwamba naamini haitakukirihi abadani.
MAHITAJI
- Maparachichi 4
- Ndizi 3
- Maziwa nusu Lita(500ml)
- Sukari kiasi
- Vanilla/ice cream flavour (sio lazima)
MATAYARISHO
- Katakata Maparachichi na ndizi vipande vipande
- Weka mahitaji yote kwenye blender na ublend mpaka kila kitu kichanganyike na kusagika vyema
- Mimina kwenye jagi au sehemu yeyote ueke kwenye jokofu ishike baridi
- Andalia familia muda mchache baada ya kula chajio kama kitindamlo.
KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA
- Instagram @farwats_kitchen
- Facebook@farwat’s kitchen
- You tube@farwat’s kitchen