
MAHITAJI
- Mikate ya pizza ya tayari (unaeza ipata supermarket)
- Kuku aliyechemshwa pamoja na chumvi na Kitunguu thomu na kutoanishwa
- Tomato 5 zilizosagwa na Kitunguu thomu na Kitunguu maji
- Vitunguu maji 3
- Pilipili boga moja
- Carrots 1 kubwa
- Mafuta ya kupikia kiasi
- Chumvi kiasi
MATAYARISHO
- Weka sufuria motoni pamoja na mafuta. Mafuta yakishika moto weka zile tomato ulizosaga na chumvi uzipike mpaka ziive kisha weka pembeni
- Weka mafuta takriban kijiko kimoja upike vitunguu, pilipili boga na carrots kwa sekunde kadhaa (zisiive) ueke pembeni
- Weka mikate ya pizza kwenye tray ya kubakia
- Paka tomato, kisha weka kuku, juu weka vitunguu, pilipili boga na carrots. Hatimaye weka cheese
- Bake Kwa Moto wa juu tu Kwa dakika kumi, kiasi cha cheese kuyeyuka Tu.
Pizza iko tayari
Andaa kwa juisi ya passion.
KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA
- Instagram@farwats_kitchen
- Facebook@farwat’s kitchen
- You tube@farwat’s kitchen