JINSI YA KUPIKA MISHKAKI

      No Comments on JINSI YA KUPIKA MISHKAKI

Mwezi mtukufu wa Ramadhani umewadia na kina mama wapo mbioni kutafuta mapishi mapya na mazuri ili kuandalia aila zao. Naam, kufurahisha familia bila shaka ni jambo jema kwani hujenga udugu, mapenzi na itifaki kwa kuleta watu pamoja wakati wa kufuturu. Kwa upande mwingine vile vile ni vyema zaidi kuchunga muda hasa wakati adhwimu kama huu wa Ramadhani. Hivi unajiuliza itawezekanaje kufurahisha familia kwa mapishi aina aina na kuchunga muda Kwa wakati mmoja?  Bila shaka inawezekana. Sio lazima kuketi jikoni asubuhi mpaka jioni, kisa unaandalia familia futari, la hasha! Yapo mapishi ambayo kwamba ni rahisi sana kupika na yanachukua muda mchache kabisa, al muhimu ujipange vyema tu. Miongoni mwayo ni mishkaki. Ungana nami tujifunze kupika mapishi haya kwa njia rahisi.

MAHITAJI

 • Nyama ya ngombe(steki) kilo 1 iliyooshswa na kukatwa vipande vidogo vidogo
 • Ukwaju kiasi ulooroweka Kwa dakika kadhaa na kuukamua mzito mzito kisha ukauchuja
 • Kitunguu thomu kilichosagwa pamoja na tangawizi vijiko 2 vya mezani
 • Pilipili manga kijiko 1 cha mezani
 • Mutton masala kijiko 1 cha mezani
 • Paprika kijiko 1 cha mezani
 • Mafuta uto vijiko 2 vya mezani
 • Limau/ndimu 2
 • Chumvi kiasi
 • Vijit vilivyorowekwa kwenye maji (ili visiungue)

MATAYARISHO

 • Weka viungo vyote kwenye nyama uchanganye vizuri kisha iweke kwenye kibakuli ufunike vizuri na uiache Kwenye friji usiku kucha(au masaa 6 na zaidi) Bakisha ukwaju kidogo uloutia viungo, utaihitajika mbeleni.
 • Itoe kwenye friji tayari kuchomwa
 • Weka vipande takriban vinne kwenye kila kijiti
 • Weka nyama yako kwenye chuma cha kuchomea na uweke juu ya jiko la makaa (unaweza ukatumia oven na ukatumia moto wa juu. Pia hakikisha tray ya oven unaiweka maji kisha ueke chuma ulichoeka mishkaki juu yake ili mishkaki isikauke)
 • Choma upande mmoja Kwa dakika 5 kisha paka ule ukwaju ulobakia juu yake
 • Geuza upande wa pili upake ukwaju upike Kwa dakika 3
 • Mishkaki ipo tayari
 • Iweke kwenye aluminium foil mpaka wakati wa kuandaa
 • Andalia familia kwa chips

KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA

 • Instagram@farwats_kitche
 • Facebook@farwat’s kitchen
 • You tube@farwat’s kitchen

❤❤❤

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *