
MAHITAJI
- Njugu robo kilo(1/4 kg) zilizosagwa vizuri
- Sukari kikombe 1 &1/4
- Maji kikombe 1
- Iliki kiasi
- Vanilla kiasi(sio lazima)
MATAYARISHO
- Weka maji na sukari kwenye sufuria ubandike motoni na uache Kwa takriban dakika 10 mpaka ianze kunata
- Weka vanilla na iliki ukoroge na uache Kwa sekunde kadhaa
- Weka njugu ukoroge Kwa takriban dakika 2_5( mpaka zianze kuachana na sufuria)
- Zibandue motoni na uzimimine katika sehemu uliopaka mafuta uto(mafuta ya kupikia), unaweza ukatumia kibao cha chapati, nyuma ya sinia au hata kwenye baraza
- Zitandeze vizuri (unaweza ukatumia kigongo cha kusukumia chapati ulichokipaka mafuta kuzitandaza)
- Zikate katika shape ya almasi na uziwache zipoe
- Zitoe na uziweke kwenye sahani
- Andaa kwa kahawa
KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA
- Instagram@farwats_kitchen
- Facebook@farwat’s kitchen
- You tube@farwat’s kitchen
❤❤❤
Yummy 😋