JINSI YA KUPIKA SAMBUSA ZA NYAMA

      2 Comments on JINSI YA KUPIKA SAMBUSA ZA NYAMA

MAHITAJI

 • Kima(nyama iliosagwa) nusu iliyochemshwa pamoja na thomu(kijiko 1 cha mezani) na chumvi kiasi na kuachwa ikauke maji kabisa
 • Vitunguu maji 4 vikubwa vilivyokatwa katwa vidogo vidogo(in cubes)
 • Pilipili boga (hoho) 1 iliyokatwa katwa ndogo ndogo
 • Dania 1
 • Mdalasini kijiko 1 cha chai iliyosagwa
 • Pilipili manga kijiko 1 cha chai iliyosagwa
 • Bizari nyembamba/jira kijiko 1 cha chai iliyosagwa
 • Dania ya unga kijiko 1 cha chai
 • Currypowder kijiko 1 cha chai
 • Ndimu/limau 1
 • Kima/Manda(unaweza ukanunua za tayari kwenye bakery au ukatengeza mwenyewe nyumbani)

MATAYARISHO

 • Weka viungo vyote(spices) kwenye kima uliyoichemsha na uipike Kwa sekunde 20_30(usipike sana ili viungo visipoteze harufu yake) kisha uiache ipoe
 • Iinike nyama ya kima kwenye sinia au sahani kubwa kisha weka vitunguu maji, pilipili boga na dania na uchanganye vizuri
 • Tayarisha unga wa kufungia sambusa ambapo utaeka unga takriban vijiko 4 na maji kidogo kisha ukoroge vizuri (hakikisha hauwi mwepesi sana au mzito Sana)
 • Chukua manda moja ukunje uache nafasi ya kueka nyama. Weka nyama kisha uendelee kuifunga yote huku ukipaka ule unga ulokoroga kwenye maji ili manda igande
 • Fanya vivyo hivyo kwa manda zote
 • Bandika mafuta motoni uyaache yashike moto kidogo (hakikisha hayashiki moto sana kwasababu yatafanya sambusa zitoke pele)
 • Mafuta yakishika moto, weka sambusa uzikaange mpaka ziwe na rangi ya hudhurungi
 • Toa sambusa kwenye mafuta na uziweke kwenye bakuli la kuchuja mafuta
 • Sambusa zipo tayari

MAELEZO MUHIMU

 • Ikiwa umeweka sambusa mbichi kwenye freezer zikashika donge na unataka kuzichoma, zichome hivyo hivyo na donge lake kwasababu ukiziacha ziyeyuke zitapasuka suka. Ziache ziyeyuke kwenye mafuta zitatokea sawa tu

KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA

 • Instagram@farwats_kitchen
 • Facebook@farwat’s kitchen
 • You tube@farwat’s kitchen

 

 

2 thoughts on “JINSI YA KUPIKA SAMBUSA ZA NYAMA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *