JINSI YA KUPIKA SAMAKI WA KUPAKA

      No Comments on JINSI YA KUPIKA SAMAKI WA KUPAKA

MAHITAJI YA SAMAKI

 • Samaki mmoja mkubwa aliyesafishwa vizuri na kupigwa mitai(kukatwa mistari ili viungo viingie vizuri)
 • kituKitu thomu kijiko 2 cha mezani
 • Pilipili manga iliyosagwa kijiko 1 cha mezani
 • Fish masala kijiko 1 cha mezani
 • Ndimu/limau 1
 • Chumvi kiasi
 • Mafuta uto ya kumpaka samaki

MAHITAJI YA TUI

 • Tui zito vikombe 3
 • Currypowder kijiko 1 cha mezani
 • Pilipili manga iliosagwa kijiko 1 cha mezani
 • Mdalasini iliosagwa kijiko 1 cha mezani
 • Kitunguu thomu kijiko 1 cha mezani
 • Chumvi kiasi

MATAYARISHO

 • Changanya viuongo vyote vya samaki  kisha umpake samaki viungo hivi
 • Mpake samaki mafuta uto kidogo juu ili asishike kwenye chuma wakati wa kumchoma(mpake Kwa tahadhari ili viungo visitoke)
 • Mueke samaki kwenye chuma na umchome kwenye makaa. Akishaiva upande mmoja utamgeuza upande wa pili taratibu ili pia aive
 • Samaki akienda kuiva, endelea na matayarisho ya tui
 • Bandika tui motoni na ueke viungo vyote vya tui
 • Koroga tui lako mpaka liwe zito Kwa takriban dakika 20(hakikisha tui ni zito Sana ili lishikane na kuwa zito haraka)
 • Epua tui lako tayari kumpaka samaki
 • Unaweza ukampaka samaki pale pale kwenye chuma ulomchomea au ukamueka kwenye chuma cha chapati umpake Kwa urahisi
 • Anza kumpaka samaki wako upande mmoja kisha umgeuze umpake na upande wa pili
 • Samaki Yuko tayari
 • Andaa mezani Kwa mkate wa mofa

MAELEZO YA ZIADA

 • Unaweza ukamchoma samaki Kwa oven pia. Utamueka kwenye chuma cha oven kisha chini ueke tray ili oven lisimwagikiwe na viungo likachafuka.

KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA

 • Instagram@farwats_kitchen
 • Facebook@farwat’s kitchen
 • You tube@farwat’s kitchen

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *