JINSI YA KUPIKA BIRIANI LA NYAMA YA N’GOMBE SIMPLE NA EXPRESS

MAHITAJI YA ROJO

 • Nyama nusu kilo(1/2 kg)
 • Kitunguu thomu kilichosagwa pamoja na tangawizi kijiko cha mezani 1
 • Pilipili manga iliosagwa kijiko cha mezani 1
 • Bizari nyembamba/jira iliosagwa kijiko cha mezani 1
 • Mdalasini iliosagwa kijiko cha mezani 1
 • Maziwa mala vijiko vya mezani 5
 • Pilipili boga 1 ilioiliokatwa katwa
 • Vitunguu maji 3 vilivyokatwa katwa slices
 • Nyanya 8 zilizoblendiwa(unaweza ukaziblend na carrots ukipenda)
 • Tomato ya mkebe/paste vijiko vya mezani 4
 • Dania 1
 • Viazi 4 vikubwa vilivyokatwa katwa size ta kiasi
 • Rangi ya viazi
 • Mafuta ya kupikia/uto kiasi
 • Chumvi kiasi

MAHITAJI YA WALI

 • Mchele nusu kilo (1/2 kg)
 • Mafuta ya uto vijiko vya mezani 3
 • Rangi ya golden yellow na green

MATAYARISHO

 • Weka nyama kwenye sufuria pamoja na mahitaji yote ya rojo isipokuwa viazi, rangi ya viazi, Kitunguu maji, dania na mafuta
 • Koroga vizuri, ubandike motoni uache nyama iendelee kuiva(unaweza ukatumia pressure cooker ndio nyama iive haraka na ilainike vizuri)
 • Kaanga Kitunguu maji mpaka kiwe golden brown kisha kiweke pembeni
 • Weka rangi ya viazi kidogo na chumvi kwenye viazi na uvichanganye vizuri
 • Vikaange viazi kwenye mafuta mpaka viive lakini visiive sana kisha viweke pembeni
 • Tizama rojo lako  na kama nyama imeiva na limekauka, weka viazi na vitunguu ulivyovikaanga, dania na mafuta uto na uliache lichemke Kwa dakika 5
 • Rojo lipo tayari
 • Endelea na matayarisho ya wali
 • Bandika motoni mchele uliouosha vizuri na kuuroweka Kwa dakika kadhaa na ufunike mpaka uanze kuiva kisha mwaga maji
 • Urudishe motoni na utie mafuta
 • Tengeza shimo upande mmoja utie rangi ya golden brown na upande mwingine utie rangi ya green
 • Funika wali wako uendelee kukauka na kuiva vizuri
 • Biriani lipo tayari
 • Andaa mezani Kwa kachumbari, pilipili ya kukaanga na juisi ya passion

KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA

 • Instagram@farwats_kitchen
 • Facebook@farwat’s kitchen
 • You tube @farwat’s kitchen

 

 

2 thoughts on “JINSI YA KUPIKA BIRIANI LA NYAMA YA N’GOMBE SIMPLE NA EXPRESS

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *