
MAHITAJI
- Mihogo 4 mikubwa iliyochambuliwa maganda, kuoshwa na kukatwa vipande vya kiasi
- Kitunguu maji 1 kikubwa kilichokatwa katwa
- Pilipili boga(hoho) 1 lililokatwa katwa
- Tomato 4 kubwa zilizokatwa katwa
- Matusha/tui jepesi vikombe 5(weka mengine pengine ya kuongezea iwapo muhogo itakuwa haujaiva)
- Tui zito vikombe 3
- Royco vijiko 2 vya mezani
- Chumvi kiasi
MATAYARISHO
- Weka muhogo na mahitaji mengine yote kwenye sufuria isipokuwa tui zito na Royco
- Bandika motoni ufunike uache muhogo uendelee kuiva Kwa takriban dakika 20(itategemea na muhogo. Mihogo mengine migumu inachukua muda zaidi)
- Funua uangalie kama muhogo umeiva. Kama haujaiva ongeza matusha
- Kama umeiva, weka tui zito ulilokoroga royco ndani yake na uache Kwa takriban dakika 5
- Muhogo upo tayari
- Andaa mezani kwa samaki, pilipili ya ndimu na juisi ya maembe
MAELEZO YA ZIADA
- Kwa wanaopenda Papa mkavu unaweza ukaongeza papa mkavu takriban vipande 10 katika hatua ya Kwanza ya kupika muhogo
KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA
- Instagram@farwats_kitchen
- Facebook@farwat’s kitchen
- YouTube@farwat’s kitchen