JINSI YA KUPIKA MAHAMRI LAINI NA MATAMU SANA

MAHITAJI

 • Unga wa ngano vikombe 4/500g
 • Sukari kikombe 1/4
 • Tui la nazi zito kikombe 1& 1/2
 • Mafuta uto/ya kupikia vijiko vya mezani 2
 • Hamira kijiko cha mezani 1
 • Iliki kijiko cha chai 1
 • Unga wa maziwa vijiko vya mezani 2

MATAYARISHO

 • Weka unga wa ngano kwenye bakuli uchanganye na unga wa maziwa kisha utengeze shimo katikati
 • Weka sukari, hamira, iliki, mafuta uto na tui na uzikoroge mpaka sukari iyeyuke
 • Changanya pamoja na unga mpaka uchanganyike vizuri. Hakikisha unga hauwi mgumu na hauwi laini sana kama wa chapati
 • Tengeza madonge ya kiasi, uyachovye kwenye unga kisha uyapange kwenye sahani, baraza au sehemu yeyote Safi uliyoimwagia unga na uyafunike. Hakikisha madonge unayapanga mbali mbali ili uyapatie nafasi ya kuumuka/kufuta
 • Yawache madonge Kwa takriban saa zima mpaka yafure vizuri. Ukitaka yafure haraka utaongeza kipimo cha hamira wakati wa kukanda
 • Bandika mafuta motoni yaendelee kushika moto
 • Sukuma mahamri na uyakate mara nne ili yawe na shape ya pembe tatu. Unaweza ukayakata mara mbili yakawa na shape ya mwezi au ukayaacha round. Ila ukitaka mahamri ya round utafanya madonge madogo madogo Sana. Pia usisukume donge Sana mpaka likawa lembamba kama chapati
 • Mafuta yakishika moto vizuri, weka mahamri yako na uyapike mpaka yawe na rangi ya kupendeza pande zote mbili
 • Yatoe kwenye mafuta uyaweke kwenye kitu cha kuruhusu mafuta kupenya
 • Andaa yakiwa moto Kwa mbaazi au chai

MAELEZO MUHIMU

 • Unga wa maziwa unasaidia mahamri kuwa laini zaidi japo si lazima
 • Kama uko sehemu ya baridi hakikisha unaweka hamira ya kutosha na unaweka madonge ya mahamri karibu na moto kwasababu joto ndilo linalosaidia mahamri kuumuka
 • Usiweke sukari nyingi kwasababu inaweza ikasababisha mahamri yasiumuke
 • Hakikisha mafuta yanashika moto vizuri ndio mahamri yafure vizuri yakiwa kwenye mafuta

KWA MAELEZO ZAIDI UTANIPATA

 • Instagram@farwats_kitchen
 • Facebook@farwat’s kitchen
 • You tube@farwat’s kitchen

❤❤❤

2 thoughts on “JINSI YA KUPIKA MAHAMRI LAINI NA MATAMU SANA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *