
MAHITAJI
- Unga wa ngano vikombe 5
- Samli ilioekwa motoni Kwa sekunde kadhaa vijiko vya mezani 3_4
- Chumvi kiasi chako
- Maji yasiokuwa moto wala baridi(at room temperature) glass 2 ndogo.
MATAYARISHO
- Weka unga kwenye bakuli uchanganye na chumvi vizuri
- Weka samli uchanganye mpaka vidonge vyote viishe
- Weka maji kidogo kidogo ukiendelea kukanda unga mpaka ushikane na ulainike vizuri.
- Funika unga kisha ueke pembeni Kwa takriban dakika 30(ukieka Kwa muda mrefu zaidi ndio utalainika zaidi)
- Funua unga wako utoe madonge matatu(size ya madonge itategemea na mahali pako pa kusukuma. Kama ni pakubwa unaweza hata ukafanya donge moja Tu)
- Sukuma donge moja moja kama chapati kisha upake mafuta na ukunje kama swissroll(kufanya tabaki)
- Gawanya size unayotaka na ukunje vizuri chapati zako
- Ziwache tena Kwa takriban nusu saa au zaidi ili zizidi kulainika
- Bandika chuma cha kuchomea chapati motoni na uache kishike moto
- Chuma kikiendelea kushika moto, sukuma chapati zako size unayotaka (zisiwe nene wala nyembamba Sana)
- Chuma kikishashika moto, weka chapati uanze kuchoma
- Chapati ikishika rangi kidogo upande mmoja,geuza upande wa pili pia ishike rangi
- Weka samli upande mmoja na uipike chapati Kwa sekunde kadhaa huku ukiemezea chini Kwa kitambara au kijiko kikubwa ili ikolee rangi nzuri. Geuza upande wa pili ufanye vivyo hivyo.
- Chapati zipo tayari
- Andaa zikiwa moto kwa maini, maharagwe au chochote upendacho.
MAELEZO YA ZIADA
- Ongeza unga wa maziwa takriban vijiko 3_4 vya mezani itasaidia chapati kuwa laini zaidi
- Weka chapati kwenye mfuko wa lailoni ili zisipoe na pia zibaki laini
- Usiiwache chapati Kwa muda mrefu kwenye moto kwasababu itakuwa kavu
- Usipike chapati Kwa Moto mkubwa Sana kwasababu itaungua kabla ya kuiva.
- Usiwache wazi madonge yako ya chapati au unga baada ya kuukanda kwasababu unaweza ukafanya ukoko juu
KWA MAELEZO ZAIDI UTANIPATA
- Instagram@farwats_kitchen
- Facebook@farwat’s kitchen
- You tube@farwat’s kitchen
nashukuru kwa maelekezo mazuri ya kupika chapati
Karibu sana ❤
Ooh asante mummy
Karibu sana❤