
MAHITAJI
- Maembe 3 mabichi
- Nyanya 5 kubwa
- Tomato paste/ tomato ya mkebe kijiko 1&1/2 cha kula
- Pilipili mbichi takriban 20
- Vitunguu maji 2
- Thomu konde 8
- chumvi kiasi
- Mafuta ya uto/ ya kupikia vijiko 3 vya kula
MATAYARISHO
- Osha vizuri mahitaji yanayohitajika kuoshwa, uchambue maganda na ukate kate vipande vya kiasi.
- Weka kwenye blender kila kitu isipokuwa tomato paste na chumvi kisha blend vizuri.
- Bandika motoni sufuria uliotia mafuta
- Mafuta yakishika moto, weka mchanganyiko ulioblend pamoja na tomato paste na chumvi ukoroge vizuri
- Funika uache itokote Kwa moto mdogo mdogo Kwa takriban dakika ishirini
- Funua uone kama ishakauka, kama bado ifunike tena uiache mpaka ikauke vizuri.
- Pilipili ipo tayari. Andaa Kwa pilau, biriani, wali mweupe au chochote upendacho.
MAELEZO YA ZIADA
- Hakikisha unachanganya maembe mabichi na yalioiva kidogo ili pilipili isiwe chachu/Kali sana
- Kama maembe yako yote ni mabichi sana, basi utaongezea na sukari kidogo kama nusu kijiko cha kula.
- Kama unataka pilipili yako ikae kwa muda mrefu bila kuharibika, weka mafuta mengi.
- Unaweza ukaongeza achari ya maembe/ ya mbirimbi wakati wa kupika pilipili hii ili ilete ladha tofauti tofauti.
KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA
- Instagram@farwats_kitchen
- Facebook@farwat’s kitchen
- You tube@farwat’s kitchen