
MAHITAJI
- Kuku nusu aliyeoshwa, kukatwa katwa, kukaushwa maji vizuri na kukatwa mistari(mitai) ili spices ziingie vizuri
- Thomu iliyosagwa kijiko 1 cha mezani (1tbspn)
- Paprika kijiko 1 cha mezani
- Chicken masala kijiko 1 cha mezani
- Pilipili manga iliosagwa kijiko 1 cha chai
- Ndimu/limau moja
- Bread crumbs kiasi
- Yai moja
- Chumvi kiasi
- Mafuta ya uto ya kukaangia kuku
MATAYARISHO
- Weka Kuku kwenye bakuli utie thomu, paprika, chicken masala, pilipili manga, maji ya ndimu/limau na chumvi kisha changanya vizuri umueke pembeni Kwa takriban nusu saa au zaidi
- Bandika mafuta motoni yaendelee kushika moto
- Changanya lile yai moja pamoja na chumvi
- Chukua kipande kimoja kimoja cha kuku utie kwenye mayai kisha kwenye bread crumbs na hatimaye kwenye mafuta yalioshika moto.
- Hakikisha mafuta hayashiki moto sana na pia wakaange kuku Kwa Moto mdogo mdogo ili waive vizuri ndani na wawe na rangi nzuri
- Wakishashika rangi nzuri na kuiva upande mmoja wageuze upande wa pili
- Watoe kwenye mafuta na wako tayari kuliwa.
- Andaa mezani Kwa chips.
MAELEZO MUHIMU
- Bread crumbs unaweza ukazipata supermarket
- Hakikisha kuku ukimtia kwenye mayai unamtoa hapo hapo(immediately). Ukimuacha kwenye mayai kwa muda mrefu, spices zinaweza toka kwenye kuku.
- Hakikisha kuku unamkausha vizuri sana baada ya kumuosha ili asitoe maji wakati unatia spices.
KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA
- Instagram@farwats_kitchen
- Facebook@farwat’s kitchen
- YouTube@farwat’s kitchen