
MAHITAJI
- Unga wa dengu kikombe 1
- Mayai 5 yaliochemshwa na kukatwa slices tatu tatu
- Pilipili boga/hoho 1 lililokatwa katwa vipande vidogo vidogo
- Kitunguu maji 1 cha kiasi kilichokatwa vipande vidogo vidogo
- Thomu iliosagwa kijiko 1 cha chai
- Baking powder kijiko 1 cha chai
- Chumvi kiasi
- Mafuta ya uto/ ya kupikia kiasi cha kukaangia bajia
- Maji kiasi
MATAYARISHO
- Weka mahitaji yote kwenye bakuli isipokuwa mafuta, mayai na maji
- Anza kutia maji kidogo kidogo mpaka mchanganyiko uwe mzito kiasi. Hakikisha unakuwa mzito kuliko wa kupikia viazi karai
- Bandika mafuta motoni yashike moto
- Chukua mayai uyatie kwenye mchanganyiko wa unga wa dengu kisha ukaange kwenye mafuta
- Zigeuze geuze bajia mpaka zishike rangi nzuri ya hudhurungi. Hakikisha unazipika Kwa moto wa kiasi ili ziive vizuri na zishike rangi nzuri.
- Bajia zipo tayari
- Andaa Kwa pilipili ya ndimu n juisi ya ukwaju
KWA MAPISHI ZAIDI UTANIPATA
- Instagram@farwats_kitchen
- Facebook@farwat’s kitchen
- You tube@farwat’s kitchen
❤❤❤