
Nashika yangu kalamu
Kutunga yangu nudhumu
kusema yalo muhimu
Ndugu zangu nisikia
Ni kuhusu almasi
Isiyo na wasiwasi
Tulioletewa sisi
Na mtume hashimia
Ni kitabu qurani
Kitabu chenye thamani
Kisicho na nukusani
Cha kutuongoza njia
Ni maneno matukufu
Yasio na upungufu
Kutoka kwake raufu
Kwetu sisi ibadia
Basi tushikeni hamu
Kukisoma Kwa nidhamu
‘tatuongoza rahimu
Na peponi kututia
Ni kitabu namba wani
Kisicho na shaka ndani
Hala hala ikhiwani
Tukisomeni kwa nia
Ni dawa hiki kitabu
Maradhi kinatutibu
Pia ukiwa na tabu
Kisome utatulia
Katu tusikipuuze
Amrize tusisaze
Tusome kituongoze
mola ataturidhia
Wanetu tuwafundishe
Pia tuwahifadhishe
Ili tuwakurubishe
Na dini isilamia