JINSI YA KUTENGENEZA PILIPILI YA NDIMU/ LIMAU NA SIKI

MAHITAJI
▪ Pilipili mbichi takriban 30 hivi
▪ Kitunguu maji 1 kikubwa
▪ Kitunguu thomu konde 5 kubwa kilichotolewa maganda
▪Limau/ndimu takriban 6 kubwa
▪Siki kiasi
▪ Chumvi kiasi

MATAYARISHO
▪Osha ndimu/limau kisha uzikamue maji
▪Katakata Kitunguu maji, thomu na pilipili mbichi
▪Weka mahitaji yote ndani ya blender pamoja na maji ya ndimu/limau na siki(siki utaweka kiasi kulingana na uzito wa pilipili unaouhitaji)
▪Blend mpaka mchanganyiko ublendike vizuri.
▪ Pilipili ipo tayari.Mimina kwenye kibakuli(kama unaiona ni nzito sana unaweza ukaongeza siki)
▪ Unaweza ukala pilipili hii Kwa Viazi karai, chips, Viazi vya nazi au chochote upendacho.

Kwa mapishi zaidi utanipata;

🔸 YouTube@farwat’s kitchen
🔸 Instagram@farwats_kitchen
🔸 Facebook@farwat’s kitchen

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *