JINSI YA KUPIKA VIAZI KARAI KWA NJIA YA KIPEKEE

MAHITAJI
▪Viazi kilo moja vilivochambuliwa maganda na kukatwa vipande vya Kiasi
▪unga wa ngano kikombe 1
▪Unga wa dengu kikombe 1
▪masala Kiasi
▪Ndimu/limau
▪Chumvi Kiasi
▪Rangi ya viazi
▪ Mafuta ya kupikia (uto) .

MATAYARISHO
▪Chemsha viazi pamoja na chumvi.
▪Vikiishaiva mwaga maji yaliozidi kisha ukamulie ndimu/limau uregeshe motoni Kwa sekunde kadhaa huku ukivirusharusha(ukivigeuza). Epua uache vipoe.
▪ Changanya masala, chumvi na maji ya ndimu/limau. Hakikisha haiwi nyepesi ili iwe rahisi kupaka viazi vyako.
▪Paka masala kwenye Viazi vyako kisha weka pembeni.
▪weka unga wa ngano, unga wa dengu, chumvi na rangi ya viazi kidogo ukoroge. Weka maji kidogo kidogo mpka unga uwe mzito. Hakikisha unga hauwi mzito Sana wala mwepesi sana.
▪Teleka mafuta motoni na uache yashike moto.
▪Weka viazi kwenye unga kisha weka kwenye mafuta na uviache kwa takriban dakika mbili.
▪Geuza upande wa pili pia uviache Kwa muda mchache.(Viazi havitachukua muda mrefu kuiva kwasababu tulivichemsha)
▪Viazi viko tayari.
▪Andaa Kwa ukwaju/chatini na juisi ya passion.

Kwa mapishi zaidi mutanipata;
🔸you tube@farwat’s kitchen
🔸 Instagram@farwats_kitchen
🔸 Facebook@farwat’s kitchen

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *