JINSI YA KUPIKA NYAMA KAVU

      No Comments on JINSI YA KUPIKA NYAMA KAVU

MAHITAJI
🍖Nyama nusu ya ngombe
🍖maziwa mala(mtindi) 5tbspns
🍖kitunguu thomu kilichosagwa na tangawizi 2tbspns
🍖paprika 2tbspn
🍖 mutton masala 1tbspn
🍖 pilipili manga 1tbspn
🍖ndimu/limau Kiasi
🍖mafuta ya uto 2tbspn
🍖 chumvi Kiasi

*JINSI YA KUTAYARISHA*
🍖Osha nyama uikate vipande Kiasi chako.
🍖weka mahitaji yote uchanganye vizuri kisha iache Kwa takriban dakika 30 au zaidi.
🍖Weka ndani ya oven ubake Kwa 250°C Kwa takriban saa moja.( Muda utategemea kama unataka nyama iwe kavu au ibaki na supu kidogo)
🍖 unaweza ukatumia makaa au gesi lakini hakikisha moto ni mdogo mdogo ili nyama iive pole pole.
🍖Pia unaweza ukatumia pressure cooker ila utatia maji kidogo. Nyama Kwa pressure cooker inalainika haraka Sana(10_20 dakika)
🍖Nyama yako iko tayari. Andaa mezani Kwa chips, mkate wa mofa au hata wali.

*MAZINGATIO*
🍖Andaa nyama ikiwa Moto Moto la sivyo itaganda na pia Itakuwa ngumu.
🍖aina za oven zinatofautiana. Nyingine zinaivisha haraka kuliko nyingine.
🍖Ni vizuri nyama hii iwe kavu au ubakishe supu kidogo sana ili viungo viingie kwenye nyama vizuri.
🍖Usiweke maji hata kidogo kama hupiki na pressure cooker.Nyama itatoa maji yake yenyewe ambayo yanatosha kuiivisha.

✔Natumai mumefaidika wapendwa. Kama muna maswali au maoni tafadhali nipateni Instagram@farwats_kitchen. Kwa mapishi zaidi, mutayapata you tube@ farwat’s kitchen.

❤❤❤

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *