JINSI YA KUPIKA BIRIANI YA SAMAKI YA KUCHANGANYA.

Biriani ni chakula maarafu sana katika kanda ya pwani. Aghalabu chakula hiki hupikwa maharusini na katika shughuli mbali mbali kutokana na urahisi wake katika kupika, kuweza kutosha idadi kubwa ya watu na pia mapenzi ya watu Kwa chakula hiki. Kuna aina tofauti tofauti za kupika biriani. Leo nitawaonyesha jinsi ya kupika biriani ya samaki Kwa njia rahisi kabisa.

MAHITAJI
👉SAMAKI
🔸Samaki vipande 6
🔸 Kitunguu thomu vijiko vya Kula 2
🔸Fish masala kijiko cha kula 1
🔸Limau/ndimu
🔸 Chumvi Kiasi

👉ROJO
🔸 Tomato 8 zilizosagwa
🔸 pilipili boga
🔸Dania 1
🔸 Kitunguu maji 4 vilivyokatwa katwa
🔸Viazi vikubwa 3 vilivyokatwa vipande vya kiasi
🔸 Maziwa mala nusu kikombe
🔸 Kitunguu thomu kijiko cha kula 1
🔸 tomato ya mkebe/tomato paste
🔸 Pilipili manga iliosagwa kijiko kidogo 1
🔸 Mdalasini iliosagwa
kijiko kidogo 1
🔸Bizari nyembamba(jira) iliosagwa kijiko kidogo 1
🔸 Biriani masala kijiko kidogo 1

👉WALI
🔸 mchele nusu kilo
🔸karafuu
🔸 Chumvi
🔸rangi ya njano

MATAYARISHO
🔸 changanya mahitaji yote ya samaki kisha uwapake samaki vizuri.
🔸Weka rangi ya njano(Orange food colouring) na chumvi kwenye viazi kisha uvikange na uvieke pembeni.
🔸Kaanga vitunguu maji vitatu katika vile vinne mpaka viwe hudhurungi.weka pembeni.
🔸Teleka mafuta motoni uwakaange samaki mpaka waive vizuri kisha waeke pembeni.
🔸Weka mafuta kwenye sufuria uweke motoni tuanze matayarisho ya rojo.
🔸Mafuta yakishika moto, weka kitunguu maji kimoja kilichobaki ukipike mpaka kiwe hudhurungi.
🔸weka kitunguu thomu na spices zote uzipike Kwa sekunde kadhaa.
🔸weka pilipili boga na dania pia uzipike Kwa sekunde kadhaa.
🔸weka tomato, tomato paste,maziwa mala na chumvi kisha ufunike uache itokote Kwa takriban dakika 10_15.
🔸Rojo likiendelea kuiva, weka mchele uliouosha vizuri kwenye sufuria na maji Kiasi kulingana na mchele unaoutumia. Weka Chumvi na karafuu na uache ukauke maji ila usiive Sana.
🔸Rojo likishakuiva na kukauka, weka Viazi ulivyovikaanga, Kitunguu ulichokikanga, samaki na juu kabisa weka wali wako Kwa tahadhari.
🔸weka rangi ya njano.
🔸Funika biriani yako na uiache iive Kwa moto mdogo kabisa kwenye gass Kwa takriban dakika 15_20
🔸kama unatumia jiko la makaa, utafunika Kwa Moto wa juu na chini.
🔸 Biriani ipo tayari.
🔸pakua Kwa kutoa wali ulioko juu ili ubakishe rojo chini.
🔸Andaa mezani Kwa kachumbari, juisi ya maembe na achari ya ndimu/pilipili ya kukaanga.

🔴Kwa mapishi zaidi, utanipata you tube, farwat’s kitchen.

Instagram:farwats_kitchen
Facebook: farwat’s kitchen

🌹🌹🌹

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *