JINSI YA KUPIKA PODINI(CARAMEL PUDDING)

Podini(caramel pudding) ni aina ya kitindamlo maarufu sana pwani na duniani kote Kwa ujumla. Vile vile ni chakula kitamu sana na kinachopikwa Kwa mahitaji machache na ya kawaida.

MAHITAJI
🔸Mayai 6
🔸Sukari vijiko vya kula 6(ya caramel)
🔸 Sukari vijiko vya kula 6(ya pudding)
🔸 Maziwa nusu lita(500ml)
🔸iliki kijiko cha kula 1/2
🔸Ice cream flavour/vanilla (sio lazima)

MATAYARISHO
🔸Chemsha maziwa pamoja na iliki uyaache yapoe.
🔸weka sukari vijiko 6 kwenye sufuria uikoroge Kwa Moto mdogo mdogo mpka iyeyuke(usiweke maji) kisha iache ndani ya sufuria ipoe.(hii ndio inaitwa caramel)
🔸weka mayai, sukari Ile vijiko 6 ambavyo hatujavitumia, maziwa na vanilla/ice cream flavour kisha blend.(hii ndiyo pudding)
🔸mimina mchanganyiko ulioblend kwenye ile sukari ulioiyeyusha(caramel).
🔸Funika aluminium foil na ubake Kwa oven Kwa saa moja Kwa Moto 200°C mpaka ishikane na kuiva. Hakikisha tray ya oven umeweka maji.
🔸itoe kwenye oven na utoe aluminium foil. Weka sahani juu ya sufuria na ugeuze sufuria ili podini iingie ndani ya sufuria.
🔸weka Kwa fridge na userve ikiwa baridi.

MAZINGATIO
🔸Oven ziko tofauti, Kwa hiyo huenda podini yako ikachukua muda mchache au muda mwingi zaidi kuiva.Hivyo basi, kila baada ya muda, itazame podini yako kama ishashikana.
🔸Unaweza ukatumia jiko la makaa.weka maji kwenye sufuria kubwa kisha weka sufuria yako ya podini ndani na ufunike juu Kwa kitu kizito.

Kwa mapishi zaidi utanipata you tube@farwat’s kitchen.

Instagram@farwats_kitchen

Facebook@farwat’s kitchen

🌹🌹🌹

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *