JINSI YA KUPIKA MAYAI YA KUKAANGA/KIMANDA

Mayai ya kukaanga au kimanda ni chakula kinachopendwa na wengi ulimwenguni kote. Kuna aina nyingi sana za kupika chakula hiki ila mimi nitawaletea aina tofauti, ya kipekee na nzuri sana.

MAHITAJI
🔸Mayai 4
🔸Viazi 2 vikubwa vilivyokatwa vidogo vidogo
🔸tomato/nyanya 3 zilizokatwa katwa ndogo ndogo
🔸 Kitunguu maji 1 kilichokatwa katwa
🔸 pilipili boga 1 lilikatwa katwa
🔸Chumvi Kiasi

MATAYARISHO
🔸Teleka sufuria uliotia mafuta motoni na yakishashika moto weka kitunguu.
🔸 Kitunguu kikiiva Tu kidogo(kisiwe hudhurungi), utatia tomato, pilipili boga Viazi,na chumvi.
🔸Acha iendelee kuiva Kwa Moto wa kiasi mpaka tomato zivurujike na Viazi kuiva.
🔸Teleka chuma cha kukaangia Mayai(frying pan) na uweke mafuta kidogo.
🔸Mafuta yakishashika moto kidogo utaweka mayai ulioyavunja na kuyapiga.
🔸Pika mayai Kwa Moto mdogo mdogo mpka yaive vizuri pande zote mbili.
🔸mayai yakishaiva utayaweka kwenye sahani kisha utandaze vile viazi juu.
🔸kimanda kipo tayari.
🔸Andaa mezani Kwa boflo, chapati, ugali au chochote utakachopenda.

Kwa mapishi zaidi utanipata you tube@farwat’s kitchen

Instagram@farwats_kitchen
Facebook@farwat’s kitchen

🌹🌹🌹

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *