JINSI YA KUPIKA MKATE WA MAYAI

      1 Comment on JINSI YA KUPIKA MKATE WA MAYAI

 

Mkate wa mayai ni chakula maarufu sana katika kanda ya pwani. Aidha ni chakula cha zamani sana kilichokuwa kikitengenezwa na mabibi zetu enzi hizo. Kadri siku zilivyozidi kusonga na zama kubadilika, nayo mapishi ya mkate huu pia yakabadilika japo si Kwa kiwango kikubwa.

Nilipokuwa bado binti mdogo niliyekuwa bado sijalijua jiko vyema, nilikuwa nikiduwazwa sana nilipomuona mama yangu au shangazi zangu wakipika mkate huu. Nilikuwa naona ni kazi kubwa mno. Nilikuwa nikitamani sana nami siku moja nijue kupika mkate huo Kwa ustadi kama wao. Penye nia pana njia ebo! Nilijifunza taratibu na hatimaye nikajua kuupika na pia nikagundua kuwa ni mapishi yalio rahisi sana. Ungana nami tujifunze kwa pamoja.

*MAHITAJI*

🍰 Mayai 6
🍰 Sukari nusu 1
🍰unga kikombe 1

🍰iliki

🍰Baking powder kijiko 1 cha mezani
🍰 vanilla(si lazima)
🍰zabibu kavu

*MATAYARISHO*
🍰Tayarisha sufuria ya Kiasi ueke karatasi chini na uipake mafuta.
🍰Weka mayai, sukari na iliki kwenye bakuli uanze kupiga Kwa mashini(mixer) mpaka mayai yafure yaani yazidi yawe mara mbili yake.


🍰Anza kuweka unga kidogo kidogo huku ukikoroga taratibu kisha weka baking powder na vanilla
🍰Weka mchanganyiko wote kwenye sufuria.
🍰Tupia tupia zabibu juu ya mchanganyiko.
🍰Bake mkate wako Kwa moto wa juu na chini kwenye jiko la makaa( hakikisha moto kwenye jiko ni kidogo sana alafu ukifinika ueke makaa ya kutosha juu ya utakachofunikia sufuria_kitasa)
🍰 unaweza ukabake kwa oven kwa Moto wa 250°C takriban nusu saa(itategemea na aina ya oven)
🍰bofya mkate wako Kwa kijiti. Kijiti kikitoka kikavu mkate upo tayari

🍰Andaa Kwa chai ya maziwa.

*MAZINGATIO*
🍰Kiasi cha mayai kitategemea na ukubwa wa mayai. Ili kupata kipimo muafaka cha mayai, yapime Kwa kile kikombe ulichotumia kupimia unga na sukari.
🍰 Sio lazima kutumia kikombe. Unaweza ukatumia chombo chochote, muhimu ni Kiasi cha mayai na unga viwe sawa na sukari nusu yake.

✔ Natumai mumefaidika wapendwa. Kwa maelezo zaidi mutanipata Instagram@farwats_kitchen na you tube@farwats’s kitchen

1 thought on “JINSI YA KUPIKA MKATE WA MAYAI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *