JINSI YA KUTENGEZA JUISI YA MAEMBE, NDIZI NA KITANGO PEPETA.

Maisha pwani bila kupata kinywaji kitamu cha kuburudisha hayasongi vizuri. Tena kiwe kinywaji kilichotengezwa Kwa ufundi kikatengezeka. Jua linapowaka na kutoa miale yake mikali, nawe jitayarishie kinywaji uipoze miale hiyo. Vipo vinywaji aina ainati vilivyozoeleka na maarufu sana pwani na ulimwenguni kwa ujumla. Hata hivyo, kupata kinywaji kilichotengezwa Kwa njia tofauti inayoleta ladha ya kipekee, ni jambo zuri Sana.

Leo nimeamua kuwaletea utengenezaji wa kinywaji hiki au sharubati hii inayotengenezwa kutumia mahitaji machache na yanayopatikana kiurahisi sokoni. Mahitaji yenyewe ni matunda yaliyo na vitamini muhimu zinazohitajika mwilini. Moja Kwa moja tuanze matayarisho❤

MAHITAJI

🔷maembe 2

🔷Ndizi 3

🔷 Cucumber (kitango pepeta) 1

🔷 Sukari kiasi

MATAYARISHO

🔶Osha matunda yako yanayohitajika kuoshwa kisha yachambue maganda na utie ndani ya blender pamoja na sukari na maji.

🔶Saga mpaka ilainike vizuri kisha chuja.

🔵Kiasi cha maji kitategemea na uzito unaouhitaji wewe mwwnyewe.

🔶Juisi ipo tayari! Iweke ndani ya jokofu(friji) na itakaposhika baridi unaweza ukaandalia familia waburudike.

✔Kwa melezo zaidi tafadhali usisahau kunitembelea katika ukurasa wangu wa you tube@farwat’s kitchen

1 thought on “JINSI YA KUTENGEZA JUISI YA MAEMBE, NDIZI NA KITANGO PEPETA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *