JINSI YA KUTENGEZA AISKIRIMU

      1 Comment on JINSI YA KUTENGEZA AISKIRIMU

Je unawaza ni kitindamlo gani utakachowaandalia wageni wako? Au ni aina gani ya bembe utakayompelekea jirani yako wakati wa Ramadhani? Au unajihisi kula aiskirimu ila hujihisi kutoka? Usiwaze sana kwasababu leo nitawaelezea jinsi ya kutengeza aiskirimu Kwa mahitaji machache na yanayopatikana kiurahisi ukiwa kwako nyumbani bila kutumia kifaa maalum.

MAHITAJI
🍦Maziwa ya maji vikombe 2
🍦Maziwa ya unga kikombe 1
🍦 Custard iliopikwa kikombe 1(custard powder 3tbspns)
🍦 Mafuta ya uto robo kikombe
🍦 sukari kikombe 1
🍦 vanilla 1tbspn
🍦cocoa/pep rose(sio lazima)
🍦njugu(sio lazima)

MATAYARISHO

🍦weka maji kwenye sufuria na custard kisha ipike mpaka ishikane iwe nzito.
🍦Subiri custard ipoe na ueke mahitaji yote kwenye blender ublend.
🍦kama unataka ya njugu utaweka njugu ulizotoa maganda ublendie.
🍦Weka aiskirimu kwenye mkebe ufunike uweke kwenye freezer Kwa takriban masaa 10 au hata usiku mzima.

MAZINGATIO
🍦Mafuta ya uto yanasaidia aiskirimu kuwa creamy na igande kama inavyotakikana Kwa aiskirimu.

Natumai mumefaidika wapendwa.kwa maelezo zaidi nipateni Instagram @farwats_kitchen na Kwa mapishi Zaidi mutanipata YouTube @farwat’s kitchen

Subscribe to Blog via Email

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

Join 68 other subscribers

About Farwat Shariff

Farwata ambaye kwamba anatumia lakabu ya ashiki wa kiswahili katika uandishi wake ni kwa sasa hivi mwanafunzi wa somo la uchumi anayeishi Mombasa, Kenya. Aidha ni mjasiriamali, malenga na mwandishi wa kiswahili anayependa na aghlabu huandika kuhusu mambo yanayotokea na kuathiri jamii. Kuandika ni faraja yangu! Watu kuburudika na uandishi wangu ni furaha yangu❤

1 thought on “JINSI YA KUTENGEZA AISKIRIMU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *